Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema leo Januari 11, 2016 amegawa vyandarua 759223 katika Kata ya Gerezani Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam, na amesema kuwa zoezi la kugawa vyandarua ni la muhimu sana kulingana na mapambano na Malaria.

Amesema kuwa Ugonjwa wa Malaria umepungua kwa kiasi kikubwa na kuongeza kuwa usafi unaofanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi unasaidia sana katika kuondoa vimelea vya mmbu.

Pia Mjema ametoa rai kwa wananchi kufuata matumizi sahihi ya vyandarua hivyo vitumike kwa jambo ambalo limekusudiwa ili viweze kuwasaidia katika kujikinga na Malaria.

Aidha, Mjema amewashukuru Simba logistics kwa kutoa msaada huo kwani utawasaidia wananchi kwa kupunguza Malaria.

Darassa awajibu waliompinga kuwa ‘hastahili taji la mwana hip hop bora 2016’
Watanzania kushuhudia michuano ya AFCON 2017 kupitia DSTV

Comments

comments