Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mji wa Dodoma ni lazima upangwe ili uwe tofauti na miji mingine hapa nchini.

Majaliwa amesema Serikali haitaki kurudia makosa yaliyofanyika kwenye miji mingine, hivyo lazima mji upangwe kama ambavyo miji mingine mikuu inapangwa.

Amesema kila eneo kutakuwa na nyumba za aina fulani. “Hatuwezi kuachia watu wajenge popote na wanavyotaka, mji unakuwa haupangiki. Na hilo ndilo kosa lililofanyika kwenye miji mingine mikubwa ambayo tunayo kwa sasa.” – Majaliwa

Amesema Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya kuhamia Dodoma imepewa jukumu la kupitia upya ‘Master Plan’ ya mji wa Dodoma na kuainisha maeneo ambako nyumba za aina mbalimbali zitajengwa.

Video: Moladi kujenga nyumba za Watumishi Dodoma
Manji Kuwatega Kivingine Wanachama Wa Young Africans