Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Simiyu, Simon Songe amesema kuwa kitendo viongozi wa vyama vya upinzani kujiunga na chama hicho ni ishara tosha kuwa Rais Dkt. Magufuli anawagusa Watanzania katika kuwatatulia kero zao.

Ameyasema hayo mkoani Simiyu alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa CCM ya sasa hivi ni mpya ukilinganisha na hapo zamani, ambapo utekelezaji wa Ilani ya chama hicho katika kuleta maendeleo unaonekana.

Amesema kuwa viongozi hao wanaohamia chama hicho hawawezi kuunga mkono shughuli za maendeleo wakiwa upinzani kwani watakuwa wanatekeleza Ilani ya CCM.

“Hawa viongozi wa vyama vya upinzani wanaohama ni lazima wajiunge na chama tawala ili waweze kutekeleza vyema Ilani yetu, kwani kwasasa tunagusa maeneo yote ya kuleta maendeleo na kutatua kero za wananchi,”amesema Songe

Jean Pierre Bemba atupwa nje mchakato wa uchaguzi Congo DRC
Mahakama yatupilia mbali madai ya upinzani Zimbabwe