Kicheche ni mnyama mdogo mwenye vituko vingi ambavyo huwashangaza watu wengi na moja ya kituko chake ni uwezo wake mkubwa wa kujamiana mara nyingi zaidi  kwa siku na wana milio maalum kila wakitaka kujamiana.

Wataalamu wa wanyama wanasema kuwa kicheche anauwezo wa kujamiana mara 26 kwa siku sawa na mtu kukimbia umbali wa 360km kwa siku.

Na anauwezo wa kuishi kwa miaka 13 tu.

Kicheche ni mnyama anayepatikana katika  sehemu ya jangwa la sahara Barani Afrika ukanda wa savana ni adimu sana  kupatikana katika  misitu mikubwa kama ya  Congo na maeneo ya pwani.

Kicheche anafanana sana na Nguchiro ana urefu wa sentimeta 60, urefu huo ukijumlisha mwili na mkia wake ambapo mkia pekee una urefu wa sentimeta 20.

Chakula kikubwa cha kicheche ni ndege, nyoka, mijusi, chura, wadudu na wanyama wengine wadogo kama panya nk.

Unaambiwa wakati wa kukabiliana na maadui mnyama huyo hutoa harufu kali kwa kujamba na kuwafanya maadui kugaili kumkamata  na wazungu humuita “Father of  stinks kutokana na harufu kali anayo toa wakati akijihami na maadui.

Pia kicheche ana tabia ya kuinua mkia wake kwa kubinua mgongo ili aonekane mkubwa baada ya kumuona adui yake  kwa lengo la kumtisha na mara nyingi hupenda kula kila wakati.

Mafao yamponza mstaafu auawa na 'House boy'
Video: Zitto 'aiteka' Chadema, Mbowe anyang'anywa ofisi ya ubunge