Nyegere ndiye Mnyama mwenye wivu zaidi hapa duniani, na chakula chake kikubwa huwa ni asali, lakini pia mnyama huyu ni mmoja kati ya wanyama wenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake na mara zote hupenda kutembea nyuma ya jike lake huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike hilo.

Wataalamu wa tiba ya jadi maarufu kama Waganga wa kienyeji maarufu kwa kutengeneza dawa ya limbwata wamesema kuwa dawa hiyo inayotumika kumfanya mtu apende zaidi na awe msikivu kwa chochote utachoambiwa na mwenza wake hutengenezwa kwa kutumia ngozi na nyama ya mnyama Nyegere ili kumfanya mtumiaji wa limbwata awe na mapenzi na wivu kama wa mnyama nyegere.

Na wivu alionao mnyama nyegere humfanya achukie sana binadamu hasa wa jinsia ya kiume kwani hudhani kuwa mwanaume huyo anaweza kumtamani jike lake.

Mbali na tabia hiyo ya wivu aliyonayo Nyegere unaambiwa kwamba nyegere ni mnyama anayeogopwa zaidi duniani kwani kiumbe huyu anauwezo wa kupamba na wanyama wakali kama vile chui, simba na nyoka wa aina yeyote ile na sumu yake ni kali sana kana kwamba akimng’ata nyoka wa aina yeyote hufa papo hapo.

Mahakama yakataa kupokea kesi kuhusu CAG na Spika, Jaji Mkuu aandika barua
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani atoa neno kwa kampuni za ulinzi binafsi, aipongeza DataVision

Comments

comments