Kampuni ya Moladi imesema ipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Tanzania na kuelekeza nguvu zake katika ujenzi wa mji wa Dodoma.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 12, 2016 na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Abeid Adballah wakati akiongea na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake Magogoni jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa kampuni hiyo inatumia teknolojia ya kisasa na ujenzi wa nyumba zake unachukua siku chache sana.

Mkurugenzi huyo amesema teknolojia yao inawezesha ukuta wa nyumba nzima kukamilika ndani ya siku sita, nyumba zinastahimili matetemeko, vimbunga na ujenzi wake unapunguza gharama za ujenzi kwa asilimia 40.

Waziri Mkuu  Majaliwa amesema Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina maeneo ambayo imeyatenga rasmi kwa ajili ya viwanja vya makazi na anaamini katika muda wa miezi miwili wanaweza kujenga nyumba za kutosha watumishi wanaotarajiwa kuhamia katika awamu ya pili.

 

Video: Mji wa Dodoma lazima upangwe – Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Tanzia: Dk Masaburi afariki dunia
Video: Mji wa Dodoma lazima upangwe - Majaliwa