Klabu ya Manchester United imeibuka kidedea mara baada ya kuitwanga Manchester City mabao 3- 2 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Etihad jijini Manchester.

Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua ilikuwa ni Manchester City iliyoanza kutikisa nyavu za Manchester United katika kipindi cha kwanza kwa kuongoza magoli mawili kwa bila.

Aidha, katika kipindi cha pili Manchester United ilibadilika kwa kufanya mashambulizi makali na kuweza kufanikiwa kupata magoli 3 – 2 dhidi ya mahasimu wao Manchester City.

Hata hivyo, Matokeo hayo yamewachelewesha Man City kutwaa ubingwa wa EPL. Magoli mawili ya Paul Pogba na moja la Chris Smalling ndio yaliyozima ndoto za Man City kutangaza ubingwa.

Video: Marufuku polisi kufyeka mashamba ya Bangi- JPM, Uraia wa Kakobe 'Utata'
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 8, 2018

Comments

comments