Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo leo amezindua programu ya umoja wa mataifa ya usambazaji wa umeme inayotekelezwa Dunia nzima ambapo kwa upande wa Afrika kuna nchi 44 zinazotekeleza mradi huo na Tanzania ndiyo kiongozi kwa nchi za Afrika. Prof. Muhongo pia amesema mradi huo unatoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani ya Tanzania kuwekeza katika uzalishaji wa umeme.

“Mpango huu umelenga kufanikiwa mwaka 2030, lakini kwa sisi Tanzania kabla ya mwaka huo tutakuwa na umeme kwa kila mtanzania na Programu hii italifanya taifa letu lijulikane duniani kwani tuna dhamira ya kumfanya kila mtu apate umeme” – Prof. Muhongo

Naibu Waziri, Jafo Atembelea Shule Iliyoungua Moto Lindi
Petitimani ni Chanzo cha Wasanii wa Endless Fame Kutofanya Vizuri- Wema Sepetu