Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina ameagiza kupimwa kwa ubora wa maji ya mito iliyopo jijini Dar es salaam ili kuweza kujua kiwango cha sumu kilichopo katika maji hayo amabayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakitiririshwa na viwanda.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es salaam, ambapo viwanda vingi vimekuwa vikitiririsha maji katika mito hiyo na kusababisha madhara makubwa kwa jamii.

Amesema kuwa lengo kubwa la upimaji wa maji ya mito hiyo ni kutaka kujua uharibifu wa maji hayo ambao umekuwa ukifanywa na viwanda hivyo ambapo jamii imekuwa ikiathirika kwa kiwango kikubwa.

“Nimeagiza Taasisi ya Bonde Wami Ruvu, Shirika la Viwango Tanzania, NEMC na Ofisi ya Mkemia Mkuu kufanya ukaguzi ili tuweze kujua ni jinsi gani ya kuweza kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kuepukana na matumizi ya maji hayo,”amesema Mpina.

Hata hivyo, kwa upande wake Meneja Maabara wa Mazingira, Wakala wa Maabara wa Mkemia Mkuu wa Serikali, Emmanuel Gwae amesema kuwa maji yanayotiririshwa katika mito  yana sumu ambayo inaua viumbe hai.

Ngeleja afunguka kwanini hakumrudishia fedha Rugemalira
Magazeti ya Tanzania leo Julai 12, 2017