Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza kuuzwa kwa ng’ombe waliokamatwa mkoani Kilimanjaro ambao wametoka nchi jirani ya Kenya na kuingizwa nchini bila utaratibu kufuatwa.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua kongamano na wadau wa ufugaji wa kuku, ambapo amesema kuwa mara baada ya kufanya ziara katika mkoa huo walikamata ng’ombe ambao walikuwa wameingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya.

“Ile mifugo tuliyoikamata kule mkoani Kilimanjaro, iliyotoka nchini Kenya nimeagiza ipigwe mnada kuanzia leo kwa sababu wameenda kinyume cha utaratibu, na kuanzia sasa natoa siku saba kwa wakuu wa mikoa iliyopo mipakani kurudisha mifugo yote iliyoingizwa nchini,”amesema Mpina

Hata hivyo, Mpina amewahakikishia wadau wa ufugaji kuku nchini kuwa serikali itashirikiana nao na kuwatengenezea mazingira mazuri ya ufugaji kwa kuwahakikishia wanapata soko la uhakiki.

Juan Mata afanya jambo kubwa kwa watoto maskini
Chelsea kumkosa N'Golo Kante wiki tatu