Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga  Mpina amewataka Wakuu wa Wilaya  kuhakikisha Wananchi wote wananshiriki kufanya usafi katika siku zinazotangazwa kwa jili hiyo la sivyo hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Naibu Waziri Mpima amesesema hayo leo Septemba 24, 2016 katika maeneo ya fukwe za kigamboni aliposhiriki katika siku ya usafi kitaifa ya mwezi wa September ambapo amesema pia fukwe za kigamboni ni chafu sana na usafi wa mazingira katika mji wa kigamboni hauridhishi.

“Pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi katika kusafisha mazingira leo fukwe ni chafu na wengine wanatuangalia tunavyosafisha huku wakiendelea na shughuli zao, Angalia wale wavuvi kwenye mitumbwi yao wanaendelea na kazi zao na wao ndo wachafuzi wakubwa huko baharini na nchi kavu. – Mpina

Hata hivyo Naibu Waziri Mpina alimpongeza mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuanzisha kampeni ya upandaji miti maarufu kama ‘’MTI WANGU’’ na kuwashauri wakazi wa jiji kushiriki Katika siku ya uzinduzi na kuahidi kuwa pamoja nao siku hiyo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa ameelezea jitihada za usafi wa mazingira katika mji wa kigamboni ikiwa ni pamoja na mashindano ya usafi wa mazingira na kuwataka wakazi wa kigamboni kuongeza jitihada za kutosha kuiweka kigamboni safi.

 

Kama ilikupita hii hapa video DC Mjema akieleza mpango wake kwa vijana kwa vijana Ilala

Waziri Mkuu aagiza uchunguzi juu ya Madaktari wanaomiliki Maduka ya dawa
Majaliwa atembelea kiwanda cha samaki TANIPESCA