Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amewataka viongozi Wilaya ya Ilala, na kote nchini kuwachukulia hatua kali watu wanaokaidi kutunza mazingira yanayowazunguka.

Mpina ameyasema hayo leo Julai 1, 2017 jijini Dar es salaam alipokuwa akishiriki katika zoezi la usafi wa kila mwisho wa mwezi.

Amesema kuwa ili kuweza kuhakikisha zoezi hilo linatimia na kuwashirikisha wananchi wote, ni lazima viongozi  wawachukulie hatua kali wananchi ambao wanakaidi kushiriki katika zoezi hilo kwani lipo kwa ajili ya  kuiokoa jamii na magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

“Ninyi viongozi mnatakiwa kuwachukulia hatua kali wale wananchi wachache wanaokaidi kushiriki katika usafi, kwani haiwezekani watu wailaumu Serikali kwa kila kitu, sisi viongozi wa juu tuleteeni wale walioshindikana ili tuweze kuwashughulikia,” amesema Luhaga.

Usiku wa Pambano: Kambi ya Horn yatamba kumpiga Pacquiao KO
Mrisho Mpoto ateuliwa kuwa balozi wa utalii