Rapa kutoka Mwanza, Biznea ameachia video na audio ya wimbo wake mpya aliomshirikisha mkali wa sauti, Shaa, wimbo uliobatizwa jina la ‘Mali ya Mungu’.

Biznea ambaye ni moja kati ya wachenguaji wanakubalika zaidi Kanda ya Ziwa alifanikiwa kulikuna sikio la mtayarishaji mkongwe wa muziki, Master Jay aliyeamua kukaa chini na kuupika wimbo huu huku akimruhusu mahabuba wake kutupia sauti ndani.

Video ya ‘Mali ya Mungu’ imefanywa na kampuni ya ‘Kwetu Studio’ jijini Dar es Salaam.

“Master Jay alisikia wimbo wangu kabla sijarekodi akaupenda, akaona kuna kitu hapa. Ingawa ni muda mrefu hahusiki sana na masuala ya production, aliamua kuikalia mwenyewe na ndio kikatoka kitu hiki,” Biznea ameiambia Dar24.

Rapa huyo ameiongeza kuwa kwake anauchukulia huu kama wimbo wake wa kwanza rasmi akiwa chini ya menejimenti yake mpya yenye lengo la kuusogeza muziki wake kwenye masikio ya watanzania wote.

Ubaguzi Wa Rangi Waundiwa Kanuni
Maafisa mifugo watakiwa kubadilika

Comments

comments