Rapa aliyetikisa mitaa na vyombo vya habari na kuzipa shida baadhi ya nyimbo za wasanii wakubwa kushindwa kufanya vizuri kwa muda, Darassa wa ‘Muziki’ amerejea tena na ‘Hasara Roho’.

Ni ngoma ambayo bado inaendeleza mtindo usio na jina maalum wa rapa huyo, ulio na mchanganyiko wa asili ya Afrika na ngano za kisasa.

Video hiyo iliyoongozwa na Hanscana, ni moja kati ya video bora za Darassa zikiwa na matukio ya uswahilini, ushuani huku zikinogeshwa na mtindo wa kucheza alioubatiza jina la ‘Kuhangaika’. Hata hivyo, mtindo huo pia uliwahi kubatizwa jina la ‘flying swag’.

Video hii inaonekana kuwavutia wengi kwani ndani ya saa chache imetazamwa zaidi ya mara 25,000.

Enjoy:

Video: Sugu ang'aka bungeni wanasiasa kuwatumia vibaya wasanii
Video: Hotuba ya Sugu yalivuruga Bunge, Waliogonganisha vyeti hawa hapa