Nguli wa hip hop Tanzania mwenye uzito wa juu kwenye tasnia hiyo (The Heavy Weight MC), Profesa Jay ameachia rasmi video ya wimbo wake wa ‘Kazi Kazi’ wenye mahadhi ya Singeli.

Video hiyo iliyochukuliwa katika maeneo ya uswahilini jijini Dar es Salaam, inamuonesha Profesa Jay ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi akijichanganya na ndugu zake wa Uswazi akiongozwa na mkali wa Singeli, Sholo Mwamba.

Video hiyo inaonesha jinsi ambavyo ujumbe wa wimbo huo uliweza kuwabadilisha wavunja sheria na kuwafanya wasalimishe silaha zao za jadi.

Enjoy!

 

Daz Baba afunguka kuhusu dawa za kulevya, adai kukandamizwa na kutengwa
Video: Bilioni 20 za Dewji zitakavyotumika kuiimarisha Simba