Raymond aka Rayvanny ameachia video ya wimbo wake alioupa jina la ‘Sugu’, ikiwa ni rap ya majigambo kutoka kwa msanii huyo ambaye anatambulika zaidi kwa uwezo wake wa kuimba.

Rayvanny ambaye aliwahi kuwa mshindi wa shindano la kurap la Super Nyota linaloratibiwa na Clouds Media Group kupitia tamasha la Fiesta akionesha uwezo mkubwa wa kurap, ametumia kibwagizo na jina la wimbo wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

Katika video hiyo, Sugu anaonekana akiwa na Rayvanny wakiteta.

 

Video: Chama kimepata pigo kubwa - Madabida
Gerard Pique: Lionel Messi Hana Mpinzani