Msanii mpya wa kike wa muziki wa kizaki kipya, Rin Marii amefungua pazia la Bongo Flava kwa kishindo baada ya kuachia audio na video ya wimbo wake rasmi wa kwanza alioubatiza jina la ‘Salaam’.

Ndani ya video ya wimbo huo iliyotayarishwa na muongozaji Destro, Rin Marii anazituma salaam zake kwa aliyekuwa tulizo la moyo wake, salaam ambazo zimebeba ujumbe wa majuto na msamaha wa dhati.

Msanii huyo wa kike anabaini thamani ya penzi alilopewa baada ya penzi hilo kuondoka. Ingawa ana uhakika maji ya mahaba ya dhati aliyoyamwaga hawezi kuyazoa tena, anaona bora azitume salaam zake angalau atue mzigo wa majuto aliyonayo kwa kueleza jinsi ambavyo kosa alilolifanya limemfunza mengi.


Mpangilio wa mashairi na uchaguzi wa maneno, utayarishaji wa wimbo mzima utakufanya kuurudia tena hususan kama uliwahi kukutwa na kilichoimbwa.

Je, ni ‘stori’ kweli? Endelea kutembelea Dar24 atafunguka yote hapa hivi karibuni.

Video: Kova ajikita katika taasisi ya maafa
Zanzibar Wajipanga Kwa 2019 AFCON U17