Kiu ya kupata ‘Kiki’ na umaarufu wa haraka imeanza kuonekana kuwa sehemu ya tishio la maisha ya baadhi ya wasanii wa kizazi hiki, baada ya baadhi yao kuanza kufanya matukio yanayohatarisha maisha yao.

Katika hali isiyo ya kawaida, rapa Kasper Knight mwenye asili ya India, amechukua maamuzi magumu katika harakati za kutafuta ‘kiki’ ya wimbo wake mpya ambao alitaka ulipotiwe na vyombo vingi vya habari duniani.

Rapa huyo ambaye amedai aliona amekosa chombo cha habari kinachoweza kumpa ‘kiki’ kubwa kwa kushuti kipande cha video ya kupromoti ujio wa wimbo wake, aliamua kujifungia nyumbani kwake na kujirekodi mwenyewe akijipiga risasi ya kweli mdomoni kisha kupost video hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook, baada ya kumaliza tukio hilo akiwa anapumua.

Katika video hiyo, rapa huyo anaonekana akijipiga risasi kwa bastola yake bila kusita, risasi iliyopita shavuni na kuacha shimo na damu nyingi.

Ni kweli msanii huyo amefanikisha kupata ‘kiki’ baada ya video hiyo ya hatari kuangaliwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya muda mfupi. Baada ya kupost video hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook, ameandika kuwa alijisikia kujipiga risasi tu kwakuwa sio mara ya kwanza kwake kusikia maumivu ya risasi.

“Hii sio kitu. Nilishapigwa risasi mara nyingi hapo kabla na hii ilikuwa kama mara ya nne kati ya mara kumi ya kipimo cha maumivu haya tangu madhara ya mwanzo,” aliandika.

“Nilionekana kama nimepoteza kidogo baada ya mlipuko. Hii ni kwa sababu masikio yangu yalikuwa yapinga kengele kwa maumivu. Ilikuwa ngumu kujikita katika sauti. Na ingawa nilihakikisha kuwa nilijipiga risasi mdomoni, bado sikuwa na uhakika kamili,” alieleza alivyojisikia baada ya tukio hilo.

Simba SC Wathibitisha Kumuwinda Ame Ally
Gabigol Akwamisha Makubaliano Ya Santos FC Na Juventus FC