Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mch. Peter Msigwa amesema kuwa kauli aliyoitoa Askofu Zachary Kakobe siku ya Jumapili katika mahubiri yake ya kuwataka viongozi wa Chadema wakatubu haiendani na heshima aliyonayo ya utumishi wa Mungu.

Ameyasema hayo jijini Dodoma alikuwa akizungumza na Dar24Media, ambapo amesema kuwa ni aibu kwa kiongozi wa dini kushangilia mapokezi ya ndege wakati watu wakipotea, wengine wakipatikana wameuawa na kupigwa risasi kwa baadhi ya viongozi.

Amesema kuwa wanapozungumzia haki za binadamu si kwasababu ya Chadema bali ni kwaajili ya Watanzania wote, hivyo anatakiwa kuelewa kuwa mabadiliko wanayoyapigania ni ya kila mmoja.

Aidha, amesema kuwa Askofu Kakobe alishawahi kutabiri mambo mengi ambayo hakuna hata moja lililowahi kutimia, hivyo amemtaka kuhubiri mambo ya haki na si ya kupendelea upande fulani ambao anaona kuna maslahi kwake.

”Ni huyu huyu Kakobe ambaye alitueleza kuwa Mrema atakuwa Rais, ni huyu huyu aliyetuambia kuwa zile nguzo za umeme pale Kanisani kwake umeme hautawaka, Ni huyu huyu anatuambia hajawahi kukutana na Lowassa wala Chadema wakati pale Mlimani City kwenye kikao cha kamati kuu alikuwepo na mimi nilimuona,”amesema Mch. Msigwa

Alvaro Morata aikacha Chelsea, aongeza nguvu Atletico Madrid
Tuchel afunguka kuhusu Neymar na Manchester United

Comments

comments