Tundu Lissu amezungumzia hali yake kiafya amesema kuwa sasa anaendelea vizuri na bado hafahamu lini anatarajia kurudi nyumbani, Tanzania kwani bado madaktari wake hawajasema ni lini atapona, na lini atarejea.

Lissu amesema kuwa kufuatia tukio la kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana tukio lililopelekea baadhi ya viungo vyake kuvunjika amesisitiza kuwa ataendelea kuwa mpinzani.

Amesema baada ya risasi 16 mwili wake umevunjwa vunjwa na kamwe hauwezi kurudi kama ulivyokuwa kabla ya Septemba 7, 2017.

”Baada ya risasi 16 na kuvunjika viungo vyangu mwili huu umepigika lakini moyo upo pale pale msimamo upo pale pale hakuna kusarenda” amesema Lissu.

Lissu amezungumza hayo kufuatia swali aliloulizwa juu ya msiamamo wake wa kukipigania chama chake cha Upinzani mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana hali ambayo watu wengi wameichukulia kwamba ni hali ya kumsinyaisha katika harakati zake za kuibua mambo na kukipigania chama chake.

Aidha Lissu anaendelea vizuri na matibabu na Mungu akimjalia aterejea nyumbani, Tanzania.

Waasi wafanya ubakaji wa halaiki, Jeshi la UN laongeza nguvu
Video: Lissu ataja sababu za kutompuuza Musiba.