Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chama Cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amesema kuwa serikali ina mkakati wa kuua demokrasia na vyama vingi kwa kununua madiwani na wabunge.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa huo ni ufisadi mbaya na haukubariki.

Amesema kuwa haiwezekani serikali ikatenga bajeti ya kununua madiwani na wabunge huku viongozi wa serikali wakipandishwa vyeo baada ya kutimiza kile walichoagizwa.

“Kwa uchunguzi tulioufanya mpaka sasa serikali imetumia bilioni kumi kwa ajili ya kununua madiwani na wabunge, hii ni hatari sana,”amesema Mtatiro

 

 

John Bocco akabidhiwa tuzo ya mwezi Januari
Okwi aendelea kutamba D'salaam