Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amesema kuwa chama hicho kimeibiwa fedha za ruzuku kiasi cha shilingi Milioni 369.37.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 10, 2017, Mtatiro amesema kuwa fedha hizo zilitoroshwa kutoka hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania January 05, 2017 na kuingizwa kwenye akaunti ya CUF inayomilikiwa na Wilaya ya Temeke yenye jina la The Civic United Front,  ambapo ametaja watu waliohusika na kuhamisha fedha hizo.

Mtatiro anasema akaunti hiyo ilihutumika kuhamishiwa kiasi hicho cha fedha haikuwahi kuiidhinishwa na Bodi ya wadhamini ya CUF ili ipokee ruzuku kutoka Serikali Kuu. Bofya hapa kutazama

MSD yawatoa hofu watanzania kuhusu hali ya dawa nchini
Bushoke aamua kufanya kilimo na ufugaji