OKOA MAISHA YA MTOTO MARIAM | Mtoto Mariam Mwema aliyefanyiwa oparesheni 10 tumboni bila nafuu yoyote, amezidi kuteseka kwa ugonjwa wa ajabu kwa zaidi ya miaka minne sasa. Kupitia kipindi cha MKASA cha Dar24 Media akiwa na mama yake na mwalimu wake, wamesimulia hali ilivyo na jinsi anavyoteseka bila matumaini ya kupona leo wala kesho.

Mariam anaishi Kawe jijini Dar es Salaam, ni mwanafunzi anayesoma kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Kawe Ukwamani, kupitia Dar24 amepaza sauti yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Mkuu wa mkoa Paul Makonda, viongozi wote na Watanzania kwa ujumla kumsaidia ili akatibiwe nje, kwani ndiyo njia pekee iliyobakia ili kuokoa maisha yake na kumuondolea mateso makubwa anayoyapata kila siku.

Ameomba kwa viongozi wote na watanzania wote akiamini kuwa yeye ni mtanzania anayeweza kusaidiwa na watanzania kwani tuna sifa ya upendo na umoja ambao ni tunu ya thamani tuliyopewa na Mungu. Hivyo mimi na wewe kwa kiasi ambacho Mungu atatugusa nacho tumsaidie Mariam kuokoa maisha yake, arudi shule na kutimiza ndoto zake. Tazama MKASA HUU kwa urefu zaidi

Marais wastaafu wa Marekani wakutana kuchangisha fedha
Lukuvi kupambana na watakaoshindwa kuwajibika