Mtoto Patrick Dickson wa mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson amefariki dunia leo Julai 3, 2018 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Taarifa za kifo cha mtoto huyo ambazo bado hazijawekwa wazi zimewashtua watu wengi wakiwemo wasanii mbali mbali.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Zamaradi Mketema ameandika

“Tumejitahidi ila MUNGU ana mitihani yake, mikono inatetemeka ila ndio ukweli, PATY AMEFARIKI!! Pumzika kwa amani baba”

Pia Tunda ambaye ni mpenzi mpya wa Casto Dickson mara baada ya kuachana na mama mtoto wake Munalove, ameguswa na kifo cha mtoto huyo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa;

“Daah RIP Patrick Mungu amekupenda zaidi”

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 4, 2018
IGP Sirro afanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi

Comments

comments