Mtoto wa marehemu, Samwel Sita ambaye pia ni msemaji wa familia hiyo na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa kuondokewa na baba yao kipenzi, mzee Samuel Sitta aliyefariki dunia nchini Ujerumani

Benjamin amesema mzee Sitta alikuwa ni Baba wa watu wote  kwani aliweza kuwasaidia watu mbalimbali katika enzi za uhai wake.

Akizungumzia sababu ya kifo cha baba yake amesema alikuwa anasumbuliwa na Saratani ya Tezi dume iliyozidi na kuanza kushambulia viungo vingine,

Amesema mipango na ratiba zingine za msiba huo inapangwa na Bunge na Serikali kwani msiba ni wa kitaifa, aidha ameongeza kuwa marehemu atazikwa Urambo kwani ndiko alikoanzia maisha yake na angependa apumzike huko.

Video: Kifo cha Mzee Sitta ni pigo kubwa sana kwa wanamsasani – Mangula

Video: Simba tumepoteza mwanachama hai – Rage

West Ham United Kubisha Hodi Stamford Bridge
Chadema watinga Mahakama Kuu 'kumlilia' Lema, wataka IGP, AG waitwe