Nchini Marekani huko, Houston, Texas mtoto wa miaka miwili, Christopher Williams Jr amefariki dunia mara baada ya kujipiga risasi kichwani kwa bunduki ambayo imekuwa ikihifadhiwa na wazazi wake nyumbani kwao.

Tukio hilo limetokea pindi wazazi wa mtoto huyo wakiwa nyumbani, hivyo bado haijafahamika iwapo wazazi wa mtoto huyo watashtakiwa kwa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo Polisi wa Houston wamesema wanajaribu kubaini ni vipi mtoto huyo aliyepewa jina la utani “Junior” aliweza kuifikia bunduki hiyo.

Polisi wanasema bunduki hiyo ambayo hutumia risasi za ukubwa wa 9mm ilipatikana eneo la tukio na kwamba ilikuwa inamilikiwa na babake.

Aidha kumekuwa na matukio kama hayo yanayokea mara kwa mara kwa watoto kujipiga risasi na kujiua kimakosa nchini Marekani miaka ya karibuni.

Mkuu wa kitengo cha waathiriwa maalum katika idara ya polisi ya Houston David Angelo ametoa wito kwa wazazi walio na bunduki kuchukua tahadhari zaidi.

“Ni lazima uweke salama silaha, iwe ni kwa kuhakikisha kifaa cha kufyatulia risasi kimewekwa salama au kuiweka salama silaha kwa njia nyingine kuhakikisha matukio kama haya hayatokei tena siku za usoni,” alisema.

Kenedy kupimwa afya leo
Kitaeleweka ndani ya saa 48 zijazo