Mtu mrefu kuliko wote jijini Dar es salaam, Julius Charles amesema kuwa anapata changamoto kubwa sana katika namna ya kuendesha maisha yake kulingana na jinsi alivyo.

Amesema kuwa changamoto kubwa ni usafiri na maisha anayoishi mtaani kwake kwani watu wengi wamekuwa wasumbufu huku wengine wamekuwa wakimshangaa.

Amesema kuwa watu wengi sana wamekuwa wakimuuliza maswali mengi sana kitu ambacho muda mwingi kimekuwa kikimpa shida kubwa zaidi.

“Usinishangae sana urefu huu nilionao, mimi ni kijana mdogo sana, nina umri wa miaka 21, lakini napata shida sana jinsi watu wanavyo nishangaa kwa jinsi nilivyo, na wananihoji maswali mengi,”amesema Charles

Video: Maandamano mtandaoni yaikosesha usingizi Serikali, JPM ataka amani, maendeleo
Emmanuel Mbasha azidi kuweweseka, adai Flora anambania

Comments

comments