Msanii wa muziki wa bongo fleva, Diamond Platinumz ambaye hivi karibuni anatarajia kufungua studio ya Wasafi redio na Wasafi televisheni, mchakato wa kufanya uzinduzi huo upo mbioni kukamilika kufuatia hatua kubwa ambazo tayari amekwisha zifanya na nyingine kuwa zimekamilika.

Hivyo kupitia mitandao yao ya kijamii wameweza kuonesha muonekano wa ndani wa studio hizo za kisasa na vifaa vyake.

Mnamo Februari 26. 2018, Diamond akifuatana na baadhi ya wenzake toka kundi hilo la Wasafi walisafiri mpaka Zanzibar kwa lengo la kukabidhiwa leseni rasmi ya TV na Redio ya Wasafi, ambapo walikabidhiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh Rashid Ali Juma wa Zanzibar.

Hata hivyo Diamond ametangaza kuwa ufunguzi wa vyombo hivyo vya habari umelenga hasa kuinua sanaa ya Tanzania ili ikapate kuonekana kwa watu wote, lakini pia umelenga kutengeneza ajira kwa vijana wakitanzania na amekwisha anza kutangaza vijana wenye vipaji mbalimbali vya kutangaza wajitokeze ili waweze kuajiliwa katika chombo chake cha habari.

Angalia video ikionesha studio za Wasafi.

 

Jeshi la Polisi lakanusha kuhusika na kifo cha mfanyabiashara
Rais Putin kuteta na Trump kwa mara nyingine