Mfanyabiasha na Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Yericko Nyerere amesema kuwa, Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba ana ajenda nyuma ya pazia.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa ni lazima Musiba akathibitishe tuhuma hizo mahakamani.

Amesema kuwa watu kama hao wapo wengi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo wamekuwa wakifanya matukio ya kudharirisha watu mtaani na kutunukiwa vyeo.

“Unajua watu kama hawa wapo wengi sana ndani ya UVCCM, sasa huyu anataka kupata cheo, sasa nampeleka mahakamani ili liwe fundisho kwa wengine,”amesema Yericko

Mtibwa Sugar yatoa sita Ngorongoro Heroes
Mashabiki wa Arsenal waanzisha vuguvugu la kumng'oa Wenger

Comments

comments