Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba amewataka Watanzania kukataa kutumiwa na watu ambao hawalitakii mema taifa.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao kazi yao kubwa ni kuichafua serikali.

Amesema kuwa watu hao wamekuwa na tabia za kuchafua mataifa mbalimbali kwa lengo la kuharibu amani ili waweze kutimiza malengo yao.

“Niwaombe Watanzania wasikubali kutumiwa na watu wenye nia mbaya na nchi yetu, kwani watu hawa wamekuwa ni chanzo cha machafuko katika nchi nyingi hasa za Kiafrika,”amesema Musiba

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 20, 2018
Hotuba ya Rais wa TFF alipozungumza na wahariri wa habari za michezo