Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amesema kuwa anajipanga kumburuza mahakamani, Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba baada ya kumtuhumu kuwa ni mtu hatari kwa usalama wa taifa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa amekusudia kufanya hivyo ili kukomesha tabia za watu kama hao za kuzusha vitu ambavyo si vya kweli.

Amesema kuwa Musiba anatakiwa akaithibitishie mahakama kutokana na tuhumu alizozitoa kwa Mwenyekiti huyo wa kamati ya uongozi.

Aidha, siku za hivi karibuni Musiba alitaja orodha ya watu kumi ambao alidai kuwa ni hatari kwa usalama wa taifa akiwemo Julius Mtatiro.

“Nadhani huyu Musiba ametumwa, unajua kumtaja mtu kwamba ni hatari kwa usalama wa taifa, unamuweka katika mazingira magumu ambapo anaweza kutekwa ama kuuliwa,”amesema Mtatiro

Video: Mbowe awataja waliomtuma Musiba
TANNA yalaani vikali shambulio kuuawa kwa muuguzi Bugando

Comments

comments