Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume ameendelea kuukosoa Muswada wa  wa Sheria ya Vyama vya Siasa akisema kuwa una makosa mengi.

Akizungumza na Dar24 Media jijini Dar es Salaam, Fatma amesema kuwa imewalazimu kujitokeza kuupinga muswada huo kwakuwa ukipitishwa utakuwa na madhara makubwa kwa Taifa.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kupewa elimu kuhusu muswada huo ili waweze kuelewa madhara ambayo yanaweza kujitokeza kama utapitishwa.

Rais huyo wa TLS, amefafanua kuwa kitu kikubwa wanachopigania ni demokrasia kwakuwa muswada huo una vipengele vingi ambavyo vinakandamiza uhuru na haki ya vyama vya siasa.

”Kwakeli sisi sio kwamba tunaupinga muswada huu, lakini tunachotaka ufanyiwe marekebisho kwenye vipengele vyote vyenye matatizo,”amesema Fatma Karume.

Fatma Karume kupitia TLS amekuwa akiungana na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali pamoja na wanaharakati kuendesha midahalo na makongamano kuhusu Muswada huo.

Angalia video hapa chini kuangalia mahojiano kamili kati ya Fatma Karume na Dar24.

Mgonjwa amuua mgonjwa mwenzake hospitalini, ajeruhi wauguzi
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 28, 2019