Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa hata kama muswada wa sheria ya vyama vya siasa ni mbaya, ni lazima ujadiliwe na kuchangiwa maoni.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa Kongamano la kujadili muswada huo lililoandaliwa na CCM, ambapo amesema kuwa kuna baadhi ya watu na wanasiasa wamekuwa wakieneza propaganda kuhusu muswada huo.

Amesema kuwa kama muswada huo utajadiliwa na kutolewa maoni ya pamoja kati ya wananchi na wanasiasa utaweza kuleta tija kubwa katika ustawi wa demokrasia nchini.

”Muswada huu uwe mbaya au mzuri ni lazima ujadiliwe na kutolewa maoni ili tuweze kuuboresha ili uwe bora, ndio maana tunafanya makongamano kama haya, tusiishie kuambiwa mbaya, wala msiiguse, muswada huu ni harama kama nyama ya Nguruwe, msiwasikilize hao wapotoshaji,”amesema Polepole

 

Asasi za maendeleo zatakiwa kuwa chachu kwa vijana
Video: Nchi iliyopiga marufuku unene uliopitiliza

Comments

comments