Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe ametengua nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) iliyokuwa ikishikiliwa na Dionizi Malinzi na kuvunja bodi yote ya BMT.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema amefikia hatua hiyo mara baada ya kutoridhishwa na mwenendo mzima wa usimamizi wa michezo nchini.

“Nimefikia hatua hii mara baada ya kujiridhisha kuwa Baraza hili la michezo limekuwa na mwenendo mbaya katika kuongoza mpira wa miguu hapa nchini, kwani kumekuwepo na uongozi wa kibabe na kutokujali maslahi ya taifa,”amesema Mwakyembe.

Video: Mbowe azumgumza baada ya Mdee kuachiwa kwa dhamana
Mtoto wa Jay Z achanika ndani ya 4:44, Msikilize hapa