Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema anavutiwa na utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa wa  Dar es salaam, Paul Makonda anaoendelea nao katika kuwatumikia wananchi ili kuweza kujiletea maendeleo katika jamii.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipotembelea katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa kwaajiri ya kubadilishana mawazo na kushauliana katika masuala mbalimbali ya kiuongozi.

Mwakyembe amesema kuwa wao kama Wizara wanafanya mabadiliko ya sheria kwa kuunda divisheni maalumu ya Mahakama Kuu kushughulikia masuala ya rushwa na ufisadi ili kuweza kutokomeza kabisa ufisadi nchini.

“Mahakama ya kushughulikia Mafisadi na wahujumu Uchumi teyari imeshaanza kufanya kazi na tunataka kukomesha kabisa udokozi wa mali za umma”amesema Mwakyembe.

Picha 9 za michezo zitakazokuacha mdomo wazi mwaka 2016
Mpina afanya ziara ya kushtukiza Bandari ya Dar es salaam