Mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu amemtakia kheri mpinzani wake katika uchaguzi huo, Maulid Mtulia wa CCM.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Dar24 hivi karibuni, Mwalimu amesema kuwa Ukawa haiwezi kuyumba kwa sababu ya Mtulia kuhamia CCM ingawa alipigiwa kampeni na umoja huo na kufanikiwa kuwa mbunge wa jimbo hilohilo mwaka 2015.

“Kuondoka kwake yeye hakumaanishi kwamba sasa waliobakia wote hawafai. Au kwamba waliobakia wote ni kama yeye. Alikuja akakuta dhamira ya vyama, akapiganiwa akapewa fursa na akaicha… Sisi tunamtakia kila la kheri huko aliko. Sisi tunaendelea kubaki na Watanzania,” Mwalimu ameiambia Dar24.

Kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo kama ilivyo katika jimbo la Siha zinaendelea. Vyama vyote vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha vinawashawishi wapiga kura kuwapa ushindi katika uchaguzi huo mdogo wa Februari 17 mwaka huu.

Masauni atoa ufafanuzi kuhusu askari wanojichukulia sheria mkononi
Mawaziri 6 wawekwa kikaangoni bungeni