Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema kuwa kuna mapungufu makubwa sana katika sekta ya uwekezaji nchini yanayosababishwa na kushuka kwa thamani ya bidha za mazao zilizokuwa zikizalishwa hapa nchini.

Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Viwanda Biashara na uwekezaji, amesema kuwa kutokana na mapungufu hayo uwekezaji hauwezi kufanikiwa nchini.

Bashe amesema ni lazima kuwepo na uwezeshaji wa kutoa kipaumbele kwa wakulima na wafanyabiashara ili kuweza kuunganisha mfumo huo kufanyakazi kwa pamoja ili kuweza kuufikia uwekezaji huo unaohitajika.

“Nasema hivi Mwijage hata ahubiri vipi afanye lolote hataweza kufanikiwa katika hili, azunguke dunia nzima kutafuta wawekezaji lakini hataweza kufanikisha uwekezaji huu tunaoutaka,”amesema Bashe.

Video: Serikali imepiga hatua kubwa katika uwekezaji-Mwijage
Video: Polisi yataja mtandao wa ujambazi Kibiti, Meya, Viongozi wa dini sasa kushtakiwa