Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti mtendaji wa kampuni za IPP, Dkt. Reginald Mengi umewasili jioni ya leo Jumatatu Mei 6, 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Mwili wa mfanyabiashara huyo umewasili ukiwa katika ndege ya Emirates ukitokea Dubai, Falme za Kiarabu na kupokewa na mamia ya wananchi wakiwemo viongozi mbalimbali.

Mengi alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi Mei 2, 2019.

Kesho mwili wa mfanyabiashara huyo utaagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na utapelekwa nyumbani kwake Kinondoni na Jumatano Mei 8, 2019 utasafirishwa kuelekea kijijini kwake Nkuu, Machame mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika Alhamisi Mei 9, 2019.

Tazama hapa kujionea ilivyokuwa katika mapokezi yake;

 

Video: Mazito ya Mengi, Dar yazizima
Video: Lazima tujijengee tabia ya kupenda kulipa kodi- Wakili Manyama