Leo Novemba 10, 2016 mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta umewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Dar es salaam ambapo Makamu wa Rais, Samia Suluhu ameongoza waombolezaji kuupokea.

Baada ya mwili wa Spika mstaafu, Samuel Sitta kupokelewa umepelekwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam ambapo hapo kesho asubuhi Viongozi Pamoja na wananchi watatoa heshima zao za mwisho za kuuaga mwili wa marehemu katika ukumbi wa Karimjee jijini.

Mzee Sitta alifariki Novemba 7, 2016 katika Hospitali ya Technical University of Munich Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu ya saratani ya tezi dume.

Video: Nchi iko hatarini kuwa jangwa - Makamba
Breaking News: Moto mkubwa wazuka Kiwandani (Video)