Mzee Athuman Mchambua (76) mkazi wa Mtoni Mtongani jijini Dar, ambaye ameweka tangazao maeneo ya nyumbani kwake kuwa anatafuta mke wa kuoa amesema sababu za uwamuzi wake huo wa kutangaza kutafuta mke ni kutafuta wasaidizi ambao atasaidiana nao katika shughuli mbali mbali na ndiyo sababu ameweka na vigezo 6 vya mwanamke anayemtaka katika tangazo hilo.

Amesema sifa za mke anayemhitaji zimetokana na wanawake wengi kwa sasa kutokuwa waaminifu, hivyo ameamua kufanya utaratibu huo ili kila mmoja ajue kwamba anaenda kuolewa na mtu wa aina gani.

Mzee Mchambua amesema hayo wakati akifanya mahojiano na Dar24.co nyumbani kwake Mtoni Mtongani, Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa hadi sasa amepigiwa simu nyingi pia tayari ameshafanya mahojiano na wanawake wanne ambao kwa bahati mbaya hawakukidhi vigezo hivyo. Tazama hapa video

Lowassa atumia Sikukuu ya Maulid kutoa ya moyoni kwa Wananchi, Watawala
Fahamu jinsi amabvyo kula kupita kiasi husababisha vidonda tumboni