Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa anaiamini mahakama lakini uvumilivu umemshinda kulingana na kutotenda haki.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wananchi wenye kesi mbalimbali, ambapo amesema kuwa mfumo wa mahakama unahitaji kurekebishwa.

“Naimini sana mahakama lakini kwasasa uvumilivu umeNIshinda, mahakama zinasumbua wananchi masikini mpaka wengine wanapatwa na magonjwa ya moyo na wengine wanapooza na kufariki kwasababu ya kunyimwa haki yao ya msingi,”amesema Makonda.

Aidha, amesema kuwa kuna baadhi ya watendaji ambao wamekuwa wakishirikiana na matapeli kuwatapeli wananchi wanyone.

Hata hivyo, ameongeza kuwa baadhi ya watu wanajihusisha na utapeli huo tayari wameshawekwa ndani huku wengine wakiendelea kusakwa popote walipo ili haki itendeke.

Video: Kibao kingine cha Mbosso chini ya WCB ''Nimekuzoea''
Majina ya Watumishi wa Umma wanaostahili kulipwa madai ya malimbikizo ya mishahara baada ya uhakiki

Comments

comments