Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Kamishna Jenerali mpya wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike kuchapa kazi kumaliza changamoto zinazolikabili jeshi hilo.

Rais Magufuli amesema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumuapisha kamishna huyo na Balozi Joseph Sokoine ambaye ameteuliwa kuwa naibu katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

“Nakupongeza kidogo, lakini pole ndio nyingi,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemtaka Kasike kuhakikisha wafungwa wanafanya kazi ipasavyo, wazuie matumizi ya simu gerezani, washiriki katika shughuli za kilimo na ujenzi, wazuie kufanya biashara na kushiriki katika matukio ya wizi wakiwa gerezani.
 

Said Fella aanika mshahara anaolipwa na Diamond
Video: Wanaume waridhia Dangote aoe wake zao, JPM ampa pole bosi Magereza

Comments

comments