Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amesema kuwa chama hicho kimejengwa kwa misingi ya hoja hivyo mbunge wa jimbo la Mtama, Nnape Nnauye na mwenzie wa Nzega, Hussein Bashe hawawezi kufukuzwa.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Dar24Media, ambapo amesema kuwa hoja ndio zinazojenga chama imara hivyo wabunge hao hawawezi kufukuzwa kulingana na hoja zao wanazotoa bungeni.

Amesema kuwa wabunge hao hutetea wananchi na wapiga kura wao, hivyo ni wajibu wa kila mbunge kufanya hivyo kwakuwa alichaguliwa na wananchi ili awasaidie kutatua kero zinazowakabiri.

“Wabunge Nape na Bashe hawawezi kufukuzwa ndani ya chama kwa kutoa hoja ya kuwatetea wananchi na wapiga kura wake, hivyo niwatoe wasiwasi wananchi hakuna atakayefukuzwa chama,”amesema Ridhiwani

 

Kyle Walker ataja sababu za kusitisha likizo
Mabingwa wa England tangu karne ya 18

Comments

comments