Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Majura Musiba amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani kujitafakari na kujitathmini ili aweze kuchukua hatua.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania kutokea mauaji kama haya yanayoendelea kwa hivi sasa.

“Kwakweli inasikitisha sana kwa sasa, mtoto wetu Akweline ameuawa bila hatia yeyote, tukio ambalo halivumiliki, bado mauaji ya diwani wa Chadema tena ni ya kikatili kabisa yametokea, Waziri wa Mambo ya Ndani yupo tu tena amekaaa kimya, anatakiwa ajitathmini na achukue hatua,”amesema Musiba

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 26, 2018
Video: Mange Kimambi anatumiwa FBI- Musiba