Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kuna hatari ya nchi kuwa jangwa kama mabonde na mifumo yote ya mito mikuu hapa nchini isipothibitiwa kwani takribani hekari milioni moja za misitu huteketezwa kila mwaka.

Makamba amesema hayo leo Novemba 10, 2016 wakati akifanya mazungumza na dar24.com Ofisini kwake jijini Dar es salaam, amesema kuna mambo kadhaa yanayosababisha kasi ya uharibifu wa mazingira ambayo ni pamoja na, ufyekaji wa maeneo kwa ajili ya kilimo, mifugo, uchomaji mkaa na biashara ya kuni ambayo ndiyo kichocheo kikubwa cha uharibifu wa mazingira.

Aidha, Makamba amesema moja ya njia za kuokoa mazingira na kulinda hifadhi za misitu, kurejesha thamani ya maliasili, ni kupunguza ukataji  wa misitu kwa ajili ya mkaa na kubuni teknolojia za nishati ambazo ni nafuu na zenye ufanisi zaidi na endelevu ambazo zitatumika katika ngazi ya kaya.

Video: Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu miongozo na viwango vya TEHAMA
Video: Mwili wa Samuel Sitta wawasili Dar es salaam