Maafisa wakuu wa Urusi na Marekani wamejibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika ya Kusini.

Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumatatu katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa Kisoshalisti wa Venezuela, Nicolás Maduro ambaye amekuwa na mgogoro na Marekani.

Aidha, ndege hizo mbili za kivita zenye uwezo wa kusafiri mwendo mrefu bila kutua zilitua katika uwanja wa ndege wa Simón Bolívar katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas, zikiandamana na ndege nyingine mbili za Urusi.

Venezuela na Urusi zimekuwa marafiki kwa muda mrefu na ndege hizo mbili za kivita ziliwahi kutumwa tena katika taifa hilo mwaka 2008, zikiwa pamoja na manowari moja yenye uwezo wa kurusha makombora.

Hata hivyo, Waziri wa Ulinzi wa Venezuela, Vladimir Padrino amesema kuwa ndege hizo ni sehemu ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Venezuela na mshirika wake Urusi.

Jafo awapa neno TARURA
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 12, 2018