Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba amemuasa Meja Jenerali, Yakubu Hassan Mohamed ambaye ameapishwa leo Februari 15, 2018 kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Luteni Jenerali Ndomba amemtaka kiongozi huyo wa jeshi kutofanya kazi kwa kuangalia ukabila au kuwa na upendeleo wowote kwa ndugu, marafiki au imani ya dini yake na kumtaka kuwa kiongozi mwenye kutenda haki.

“Baada ya kuteuliwa tu jana inawezekana marafiki wamesema Mungu atupe nini na sisi tutafaidi hapana wewe si Mnadhimu Mkuu wa marafiki ila ujue wewe ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Wewe ni Muislam kuteuliwa kwako inawezekana Waislam wamesema na sisi tumepata hiyo siyo sahihi kwani wewe si Mnadhimu Mkuu wa Waislam bali wewe ni Mnadhimu Mkuu wa watu wa dini zote,”amesema Meja Jenerali Ndomba

Makonda awashushia neema walimu
Chadema yawasilisha malalamiko yao ofisi za NEC.