Mkazi wa Amritsar jimbo la Punjab, kaskazini mwa India, Daljinder Kaur ni mwanamke pekee aliyevunja rekodi duniani kote kuzaa uzeeni na bado anashikilia rekodi hiyo.

Ambapo katika umri wa miaka 72 alifanikiwa kujifungua mtoto wake wa kwanza na mumewe, Mohinder Singh Gill akiwa na umri wa miaka 79, mnamo April 19, 2016 na mtoto huyo alipewa jina la Armaan.

Mwanamke huyo (72) ameelezea kwamba tangu kujifungua kwake amekuwa akipata shida kiafya ambapo amekuwa akisumbuliwa na shida ya msukumo wa damu pamoja na maungio ya mwili wake kukosa nguvu.

”Nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la msukumo wa damu na nimekuwa nikiishiwa nguvu kirahisi, nimefanikiwa kuonana na madaktari walinipa dawa na kunishauri kutumia baadhi ya vyakula” alisema Deljinder”

Ni ngumu kukutana na wenzi majasiri kama hao katika dunia hii kwa uthubutu na uvumilivu walionao juu ya suala zima la kutafuta mtoto hata katika umri wao wa uzeeni.

Tazama Video hapa chini.

Mbio za baiskeli kukusanya milioni 340
Dkt. Mpango apokea ripoti ya ukaguzi wa ununuzi wa Umma