Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeitisha mkutano wa dharula wa wanasheria nchi nzima kwa ajili ya kujadili mapendekezo na kutoa msimamo wao dhidi ya Serikali ya kuanzisha Bodi ya Usajili ya Mawakili.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu alipokuwa akifungua mkutano huo.

Lissu amesema kuwa mapendekezo hayo ya Serikali kuunda Bodi ya Usajili wa Mawakili ni kutaka kuminya uhuru na haki ya mawakili pia ni hatari kwa Tasnia hiyo ya Sheria.

“Mabadiliko haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini, tumekutana hapa ili kuweza kueelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka msimamo wetu baada ya baraza la TLS kukaa,”amesema Lissu

Hata hivyo, Lissu ambaye pia ni mbunge  ameongeza kuwa mkakati huo una lengo la kuminya uhuru wa TLS katika kufanya shughuli zake za kisheria.

Ummy Mwalimu aripoti kuhusu mzazi aliyeibiwa pacha Temeke
Prof. Mbarawa afanya ziara JNIA, amhakikishia mkandarasi ushirikiano na Serikali