Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA imesema kuwa changamoto kubwa inayokumbana nayo ni baadhi ya wenyeviti wasiokuwa waaminifu ambao huwatoza fedha wananchi wanaokwenda kujiandikisha.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Rose Joseph alipokuwa akizungumza na Dar24 Media.

Amesema  kuwa kwasasa Mamlaka hiyo imejipanga vizuri kuweza kutimiza malengo yake yote iliyojipangia, hivyo wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.

 

11 waliocheza 2014 waitwa kikosini Ureno
Sethi wa IPTL avuliwa madaraka

Comments

comments